SHARE

TIMA SIKILO

KOCHA wa timu ya TP Mazembe ya DR Congo, David Mwakasu, amempeleka winga Mtanzania, Ramadhan Singano Messi anga za Mbwana Samatta.

Singano amejiunga na timu hiyo mara baada ya kumalizika kwa msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara, 2018/19 akitokea kwa Wanalambalamba wa Azam FC.
Akizungumza na DIMBA Jumatano, Kocha huyo alisema Singano ni mchezaji mzuri na mwenye nidhamu katika kila anachokifanya akimfananisha na Mbwana Samatta.

Huyu mchezaji wanamwita Messi (Ramadhani Singano) ni mzuri sana na anaweza kufika mbali kama Samatta (Mbwana) kupitia TPMazembe, alisema.
Alisema, Tanzania ina wachezaji wazuri ambao wengi hawajulikani lakini wanapopata nafasi wanaonyesha uwezo mkubwa akiwemo Eliud Ambokile ambaye kwa sasa yupo kikosi hicho na anafanya vizuri.

Samatta alipita kwenye kikosi hicho na sasa anawika akizitoa udenda timu kubwa barani Ulaya kutokana na kazi kubwa anyoifanya kwa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu nchini Ubelgiji, KRC Genk.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here