SHARE

MWANDISHI WETU

UNAMKUMBUKA yule straika hatari wa AS Vita, Jean Makusu Mundele? Basi ni kwamba bado mchezaji huyo ana ndoto za kuitumikia klabu ya Simba endapo mipango itakaa sawa.

Iko hivi, kwa sasa Mundele ni mchezaji halali wa timu ya RS Berkane ya nchini Morocco alikouzwa na AS Vita mwaka 2018 na kuanza kuitumikia mwaka uliofuata kwa mkataba wa miaka miwili.

Itakapofikia mwezi Mei mwaka huu, straika huyo atakuwa mchezaji huru na kama klabu yake haitoridhia makubaliano ya kuongeza mkataba mpya, basi atakwenda kutafuta changamoto kaika timu nyingine.

Akizungumza na DIMBA Jumatano kwa njia ya mtandao, Mundele alisema anatamani kurudi Afrika lakini zaidi akitaka kuichezea klabu ya Simba ambayo ana taarifa rafiki yake Deo Kanda aliyetokea TP Mazembe na wote raia wa DRC, anacheze.

Alisema kabla ya kupata ofa ya kujiunga na klabu yake hiyo ya sasa aliwahi kuzungumza na viongozi wa Simba, lakini hawakufikia makubaliano baada ya wakala wake kutaka akacheze soka nchini Morocco.

“Kama nitarudi Afrika, nitapenda kuichezea Simba ile ya Tanzania, kule yupo Deo Kanda mchezaji mzuri kushirikiana naye,” alisema Mundele.

Endapo Simba itatimiza ahadi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Mohamed Dewji, kuboresha kikosi cha timu hiyo kwa kutwaa ubingwa msimu huu, basi safari ya Mundele kuja Msimbazi itakuwa nyeupe kutokana uwezo wake wa kupachika mabao hususan katika mechi za kimataifa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here