SHARE

NA MARTIN MAZUGWA

STRAIKA wa Ndanda, Omari Mponda, amesema yupo mbioni kujiunga na mabingwa wa Kombe la FA, timu ya Simba ya Dar es Salaam.

Akizungumza na DIMBA, mshambuliaji huyo, aliyemaliza msimu uliopita wa Ligi Kuu Tanzania Bara akiwa na mabao sita,  amesema mazungumzo yanakwenda vizuri.

“Sikuwa sawa mzunguko wa pili kutokana na majeraha ya goti, lakini naamini uwezo wangu niliouonyesha mzunguko wa kwanza umewavutia Simba na ndiyo maana wameamua kuniita na kuanza mazungumzo,” alisema.

Alisema kuwa, anaamini iwapo atajiunga na Simba  anaweza kuwa sehemu ya mafanikio kwa klabu hiyo, yenye kiu kubwa ya ubingwa baada ya kuukosa kwa msimu mitano mfululizo, huku Yanga ikitwaa mara nne, ambapo mara tatu imetwaa mfululizo na Azam ikitwaa mara moja.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here