SHARE

NA BEATRICE KAIZA

MPENZI wa msanii wa muziki wa Bongo Fleva Diamond Platnumz Tanasha Donna, amewafunga midomo watu wote ambao wamekuwa wakimsema kuwa yupo kwenye mahusiano na staa huyo kwa ajili ya kumchuna.

Akizungumza na DIMBA,Tanasha,alisema kuwa yuko na Diamond kwa ajili ya mapenzi ya dhati aliyonayo kwani kama ni pesa hata yeye anazo za kutosha ili kuendesha maisha yake.

Naweza nisiwe tajiri lakini ninauwezo wa kutafuta pesa zangu na kujigharamia kwa chochote watu ambao wanasema nipo na Diamond kwa ajili ya pesa kitu cha kuwaambia kama pesa ninazo za kutosha na miaka ijayo naweza kuwa tajiri zaidi,”alisema Tanasha.

Kauli ya Tanasha imekuja kuwafunga mdomo baadhi ya watu kwenye mitandao ya kijamii ambao wamekuwa wakimbeza kuwa yupo na msanii huyo kwa ajili ya kumchuna na ameamua kutumia njia ya kuzaa naye mtoto ili kupiga mkwanja kilain.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here