SHARE

NA RAMADHAN HASSAN, DODOMA

UONGOZI wa timu za soka, Dundee United na Area A Sportivo za Mkoani Dodoma, zimegomea ligi ya mkoa huo huo kwa madai chama cha soka mkoani humo, (Dorefa) kina timu zake inazozipendelea ambazo zitapewa nafasi za kushinda.

Hivi karibuni Dorefa kupitia kwa Katibu wake Mkuu, Hamisi Kissoy ilitangaza kuanzisha ligi mpya kwa ajili ya kupata washindi bora wawili ambao wataungana na timu nyingine nane kushiriki hatua ya 10 bora ya Ligi ya Mkoa wa Dodoma.

Wakizungumza na DIMBA kwa Juzi viongozi hao walisema wanachokifanya Dorefa ni kuvunja  kanuni za mashindano kwani mwanzo zilionesha kutakuwa na Ligi za aina mbili kwanza itakuwa makundi na pili kumi bora.

Rashid Nyoka, Katibu Mkuu wa Dundee United alisema kamwe hawatocheza ligi hiyo na badala yake wanajiandaa na hatua ya 10 bora ya ligi nyingine inayotarajiwa kuchezwa katika Uwanja wa Mgambo Wilayani Mpwapwa.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa timu ya Area A Sportivo, Tionas Mbago alisema wanachokifanya Dorefa ni kudidimiza soka la Dodoma kwani timu ziliopata nafasi ya ‘best loser’ ziliishajulikana’’alisema

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here