SHARE

LONDON, England

KWA mujibu wa kile kilichoelezwa na kituo cha televisheni cha Sky Sports jana, staa wa kimataifa wa Misri, Trezeguet, amefuzu vipimo katika klabu ya Aston Villa.

Trezeguet, ambaye jina lake halisi ni Mahmoud Ahmed Ibrahim Hassan, si mgeni katika soka la Ulaya kwani aliwahi kucheza barani humo akiwa na Anderlecht.

Nyota huyo alikuwa kwenye kiwango bora katika fainali za Afcon 2019 zilizomalizika wiki chache zilizopita, ambapo aliweza kuingia kwenye kikosi bora cha michuano hiyo ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

Aidha, imeelezwa kuwa Aston Villa wameipata huduma yake baada ya kukubali kuweka mezani kitita cha Pauni 8,500,000 na watamtangaza hivi karibuni.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here