SHARE

NA WINFRIDA MTOI

KOCHA wa viungo wa Simba, raia wa Tunisia, Adel Zrane, ameonekana kupagawa na ubingwa wa mara ya tatu mfululizo wa Wanamsimbazi hao na kusema anajivunia mafanikio hayo.

Zrane anashudia Wekundu wa Msimbazi hao wakitawazwa kuwa mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa mara ya pili, tangu alipojiunga na kikosi hicho msimu uliopita.

Akizungumza na DIMBA, Zrane, alisema kuchukua ubingwa mara mbili na timu kubwa kama Simba ni jambo la kujivunia na historia katika maisha yake.

Alisema,kupitia Simba imemfanya kuipenda Tanzania nakuichukulia ni nyumbani kwake na kuamini kuwa mafanikio hayo yanatokana na sapoti na ushirikiano wa Wanasimba wote.

“Nimefurahi kupita kiasi tulivyomaliza mechi na kufikia pointi za sisi kuwa mabingwa,hii ni hitoria kubwa kwangu ni mara ya kwanza kuchukua ubingwa mara mbili mfululizo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here