SHARE

NA KYALAA SEHEYE

JACKLINE Wolper, mmoja wa wasanii bora katika soko la filamu nchini, amefunguka kwamba moyo wake umekufa umeoza kimapenzi kwa msanii wa muziki wa kizazi kipya, Harmonize, baada ya kupitia machungu ya kutendwa na mchumba aliyekuwa naye.

Wolper ameliambia DIMBA kwamba, Harmonize amemvusha katika kipindi kigumu alichokuwa nacho cha kuugulia maumivu ya kutendwa na mchumba wake wa zamani ambaye ni raia wa Congo DRC.

“Namshukuru Harmonize kwa namna alivyonitoa katika hali ile mara baada ya kuachana na jamaa, kwani nilikuwa nimeshakata tamaa ya maisha mara baada ya kuwekeza moyo wangu kwake, lakini matokeo yake akawa mtu katili kwangu,” alisema msanii huyo.

Alisema mchumba wake huyo amekuwa msaada mkubwa katika kumtuliza kimawazo aondokane na majeraha ya moyo na kwa hilo amefanikiwa, hivyo kwa sasa anawaza muda ufike avalishwe shela na Harmonize ili kutimiza ndoto zao za maisha.

“Nilishakata tamaa kabisa ya maisha, hata kazi nilikuwa sitaki kufanya ila kwa kuwa nina ulinzi wa kutosha kutoka kwa mpenzi wangu huyu, sina wasiwasi ninajipanga kurudi upya kwenye gemu la filamu, kwani Harmonize ameahidi kunipa sapoti.”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here