SHARE

MERSEYSIDE, England

MSHAMBULIAJI wa Everton, Richarlison, amesema uimara wa beki kisiki wa Liverpool, Virgil van Dijk, hautamzuia kuziona nyavu katika mchezo wao wa leo.

Timu hizo zitavaana katika Uwanja wa Goodison Park, mechi ya Ligi Kuu England iliyopaswa kuchezwa miezi miwili iliyopita kabla ya kupeperushwa na janga la Corona.

Alichokisema Richarlison raia wa Brazil ni kwamba ameshawahi kumvaa na kumpita Van Dijk mara kadhaa, hivyo hakuna jipya kwa mlinzi huyo raia wa Uholanzi.

“Alichaguliwa kuwa mmoja kati ya mabeki bora watatu duniani kwa kuwa alifanya vizuri msimu uliopita lakini kwangu kuna mabeki bora zaidi yake,” alisema Mbrazil huyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here