SHARE

NA JESSCA NANGAWE

WAKATI mwanadada Vanessa Mdee akiwa kwenye uhusiano mpya na staa kutoka Marekani, Rotimi amekiri wazi kuwa huwa hapendi kuwa kwenye mahusiano na mwanaume anayependa kujigamba.

Aidha Vanessa amekiri kuwa kwenye mahusiono salama na mpenzi huyo wa sasa huku akisitiza kikubwa alichofuata ni furaha ya moyo wake.

Akizungumza na DIMBA, Vanessa alisema, pamoja na kuwa kwenye mahusiano tofauti yaliyopita lakini hawezi kujutia na badala yake amesisitiza yamemsaidia kujijenga upya na kujifunza.

ìHuwa sipendi kuzungumzia mahusiano yangu ya nyuma, lakini kubwa ambalo sikuwahi kupendezwa nalo ni kuwa na mwanaume anayejigamba sana, kwangu sioni kama mtu wa hivyo ananifaa, kikubwa nashukuru nipo kwenye mahusiano salamaîalisema mrembo huyo.

Vaness ambaye kabla ya kua na Rotimi, alikua na msanii mwenzake Jux amesisitiza hata hivyo hajawahi kujutia mahusiano yakeya nyuma kutokana na kujifunza mambo mengi ambayo yanamjenga kwa sasa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here