SHARE
Gonzalo Higuain

TURIN, Italia

WAKALA wa Gonzalo Higuain, Nicolas Higuain, amesema kuwa Rais wa Napoli, Aurelio de Laurentiis, ndiye anayestahili kubeba lawama kwa kitendo cha straika huyo kuitema klabu hiyo na kujiunga na Juventus.

Nicolas Higuain, ambaye pia ni kaka wa Gonzalo, aliongeza kuwa De Laurentiis alifurahi sana kuipokea ofa ya Euro milioni 94 kwa ajili ya uhamisho huu, hivyo haoni sababu ya mashabiki kulaumu.

“Gonzalo amepokelewa vyema kule Turin. Wachezaji, benchi la ufundi na Rais wa klabu walimkaribisha kwa furaha. Juventus ni klabu inayofanya mambo haraka zaidi kuliko Napoli.

“Dunia nzima inajua Gonzalo alichokuwa anawaza na matatizo yake na De Laurentiis.

“Nashangaa watu wanapomuita msaliti, mara zote Gonzalo amekuwa akijituma na kuipambania jezi ya Napoli. Baada ya miaka mitatu ya mafanikio, tumefanya uamuzi wa kuondoka, cha ajabu ni nini?

“Napoli walijua nia ya Juve na wakaipokea. Kinachotokea sasa ni kujaribu kuficha makosa yao. De Laurentiis aliwahi kusema vibaya kuhusu Gonzalo na nina uhakika ni mwenye furaha hivi sasa kwa kupokea fedha nyingi kwa ajili yake,” alisema Nicolas.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here