SHARE

NA CLARA ALPHONCE

PAMOJA na ajenda ya mabadiliko kuwekwa kiporo mpaka Agosti 24, kwenye mkutano mkuu wa klabu hiyo uliofanyika Jumapili wiki iliyopita, klabu ya Simba leo inatarajiwa kufanya semina kubwa ya wanachama wote wa klabu hiyo.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara, katika taarifa yake jana alisema semina hiyo inalenga kujenga uelewa mpana zaidi juu ya muundo mpya wa klabu uliotokana na mabadiliko ya katiba yaliyofanywa na wanachama hao na kusajiliwa na msajili wa klabu nchini.

Alisema maandalizi yote ya semina hiyo yamekamilika na semina hiyo itaanza  saa 8.30 mchana na itafanyikia kwenye ukumbi wa Mikumi uliopo kwenye eneo la maonyesho ya kimataifa ya biashara ya Sabasaba (PTA) kurasini hapa jijini Dar es salaam.

“Tunawaomba wanachama wote popote walipo waje kwa wingi hapo kesho (leo), pia klabu inawaomba viongozi wa Simba Wilaya ya Temeke waandae utaratibu mzuri wa kuwapokea wageni,” alisema Manara.

Tayari Mohamed Dewji (MO) ameonyesha nia ya kuwekeza katika klabu hiyo kwa kuchukua hisa 51 kwa Sh bilioni 20.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here