SHARE

NA JESSCA NANGAWE

CEDRIC Kaze ameanza kuelewa upepo wa straika wake, Waziri Junior, na kukikiri kuwa ni moja ya wachezaji wanaomtia moyo sana kutokana na aina ya uchezaji wake.

Waziri Jr ambaye alitua Yanga akitokea Mbao FC iliyoshuka daraja, amekuwa na mafanikio makubwa kikosini hapo huku akiisaidia timu yake kuibuka na alama tatu mbele ya KMC baada ya kupachika bao la pili akipokea pasi nzuri toka kwa Farid Mussa.

Akizungumza hivi kakribuni, Kaze alisema amekuwa akifurahishwa na uwezo binafsi wa nyota huyo kuanzia mazoezini hadi katika mechi anazocheza hivyo kumpa ujasiri wa kumwamini zaidi.

“Waziri anacheza kwa kujiamini sana, amekuwa akitumia akili nyingi kushirikiana na wenzake na kuiletea timu ushindi, nafurahi kuona anatumia uwezo wake na kila nafasi anayopata kuipatia timu matokeo mazuri,” alisema Kaze.

Hata hivyo, Kaze amekiri kuwa anafurahishwa na uwezo wa nyota wake wote ndani ya kikosi hicho jambo ambalo anaamini litakuwa nguzo kubwa kufikia malengo.

Uelewano mzuri wa benchi la ufundi na wachezaji umeendelea kuiweka Yanga kwenye nafasi nzuri ambapo hadi sasa inakamata nafasi ya pili ikiwa na alama 19 huku ikijiandaa na mchezo ujao dhidi ya Mwadui FC.

SHARE
Previous articleKIMENUKA SIMBA
Next articleBOCCO ATULIZA UPEPO MSIMBAZI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here