SHARE

NA JESSCA NANGAWE

STRAIKA wa Mbao FC, Waziri Junior, amesema kuwa kazi yao kwasasa ni kuhakikisha wanakinusuru kikosi cha Mbao Fc kushuka daraja. Katika michezo miwili mfululizo, Mbao imefanikiwa kunyakua alama sita dhidi ya Coastal Union ya Tanga, kisha Polisi Tanzania, mchezo uliopigwa mwishoni mwa juma kwenye dimba la CCM Kirumba.

Akizungumza na DIMBA Jumatano, Waziri alisema pamoja na changamoto walizopitia lakini mipango ya wachezaji ni kupambana hadi tone la mwisho ili kuinusuru timu hiyo kubaki Ligi Kuu Bara msimu ujao.

“Tutahakikisha tunapambana hadi tone la mwisho kuibakiza timu, mipango yetu ni kushinda michezo yote iliyosalia tunashinda ili kuzidi kujiweka kwenye mazingira mazuri,” alisema Waziri ambaye hadi sasa amepachika mabao nane ya Ligi Kuu Bara.

Licha ya ushindi huo, Mbao inabaki nafasi ya 19 ikiwa na pointi 29 baada ya kucheza mechi 32 na kujikusanyia pointi 29.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here