SHARE

NA BEATRICE KAIZA

MALKIA wa filamu Tanzania, Wema Sepetu ameutaja mwaka 2009 kwamba ulikuwa mbaya kwake kutokana na skendo mbalimbali zilizompata ikiwemo ile ya kushtakiwa kwakosa la kuvuja kwa video yake akiwa faragha.

Mbali na skendo hiyo Wema ameorodhesha matukio mengine kama
kuswekwa jela wiki moja kwa kosa la kutohudhuria mahakamani lakini pia janga la kufiwa na kaka yake upande wa mama na pia kushindwa kufanya kazi kwa muda mrefu kwa ëapplication yake ya ëWemaAppí.
Akizungumza na DIMBA,alisema, amepanga ndani ya mwaka huu 2020 kufanya mambo mema ya kumpendeza Mungu.

ëíKuna mambo ambayo yalitokea mwaka 2019 kwangu yamebaki na kumbukumbu mbaya mfano ni kesi ya video ya faragha, kifo cha kaka yangu upande wa mama, kuwekwa kwa kosa la kuidharau mahakama na application yangu ya ëWemaAppí kukaa kwa muda mrefu bila ya kufanya kazi,”

“Mwaka huu 2020 kwangu nimejiwekea malengo uwe na mafanikio na kupiga kazi tu sitaki haya yajirudie tena,íí alisema Wema Sepetu.
Mwanadada huyo alisema, mashabiki zake wakae mkao wa kula kwani mwaka huu kwake ni kupiga kazi tu akiwa na mengi jikoni aliyowaandalia.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here