SHARE

AMSTERDAM, Uholanzi

ALIYEKUWA kocha wa Arsenal, Arsene Wenger, amepewa ofa ya kumrithi Ronald Koeman katika kibarua cha kuliongoza benchi la ufundi la timu ya taifa ya Uholanzi.

Kwa mujibu wa kituo cha televisheni cha Fox Sports, Koeman atatua Barcelona iliyoachana na kocha Quique Setien.

Wenger raia wa Ufaransa amekuwa nje ya taaluma ya kufundisha soka tangu alipoondoka Arsenal mwaka juzi na amekuwa akisisitiza kutamani kurejea mzigoni.

Koeman (57), anaongoza mbio za kuinoa Barca aliyowahi kuichezea kuanzia mwaka 1989 hadi 1995, licha ya mkongwe mwingine wa timu hiyo, Xavi, naye kuhusishwa na kibarua hicho.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here