SHARE

NA JESSCA NANGAWE

KUNDI la muziki wa Bongofleva la weusi linatarajia kuachia albamu yao mpya inayojulikana kama Air Weusi ambayo itakua na jumla ya nyimbo 16.

Akizungumza na DIMBA, mmoja wa wasanii wa Kudi hilo Niki Wa Pili alisema,katika albamu hiyo iliyoshirikisha zaidi ya watayarishaji wa muziki 7 itatoka hivi karibuni baada ya taratibu zake kukamilika.

ìBaada ya wiki moja tutatoa tarehe kamili ya kuachia albamu yetu mpya inayoitwa Air Weusi, hii itakua albamu ya aina yake kwa kuwa ndani yake kutakua na mambo mengi ya kiubunifu na mapya ili kuzidi kunogesha kazi zetuîalisema Niki wa Pili.

Aliongeza kuwa baada ya kauchia albamu hiyo pia wataandaa ziarambalimbali nchini kwa lengo la kuitangaza albamu yao hiyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here