SHARE

NA SAADA SALIM         | 

KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, amewaambia mashabiki wakikosi hicho wamiminike kwa wingi uwanjani leo, kwani kicheko kwao kitakuwa palepale kutokana na kipigo kikali walichowaandalia Ruvu Shooting.

Yanga ambao wapo kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu TanzaniaBara, watakuwa wenyeji wa maafande hao katika mchezo utakaochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Ruvu Shooting, hawajawahi kuondoka na pointi tatu tangu msimu wa 2010/2011, zaidi ya kuambulia sare na leo timu hizo zinashuka uwanjani huku Yanga wakitaka kuendeleza rekodi yao ya kutokupoteza mchezo wowote katika ligi.

Katika michezo hiyo, Yanga wameibuka na ushindi katika michezo 10, Ruvu Shooting wakipata sare tatu, ambapo mchezo uliochezwa Septemba 25, mwaka 2010, Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 katika mechi ya mzunguko wa kwanza, huku mchezo wa pili uliopigwa Februari 28 mwaka 2011 Yanga ikashinda tena bao 1-0. 

Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la DIMBA.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here