SHARE

Benedict TonocoNA ZAINAB IDDY

WAKATI kukiwa na taarifa za kutolewa kwa mkopo kwa kipa namba tatu wa Yanga, Benedict Tonoco, mlinda mlango huyo ameibuka na kusema kuwa hadi sasa hakuna barua yoyote aliyopewa juu ya suala hilo.

Akizungumza na DIMBA Jumatano, Tinoco, amesema hadi hivi sasa hajui hatima yake ndani ya Yanga kutokana na viongozi kutompa barua yoyote huku wakimtema safari ya Uturuki.

“Wakati nikijiandaa kurejea kikosini, nilipigiwa simu na uongozi kuambiwa kuwa nisije hadi nitakapoambiwa niende lakini hadi sasa sijui hatima yangu.

“Nafahamu kuwa wanataka kunitoa kwa mkopo lakini wanapaswa kunipa barua ili nianze kujihangaikia mwenyewe mahali pa kwenda kucheza,” alisema.

Tinoco alisajiliwa na Yanga kwa msimu wa 2014/15 kwa lengo la kuongezea nguvu nafasi ya kipa Deogratius Munishi ‘Dida’ na Ally Mustapher ‘Barthez’.

Hivi karibuni Yanga imemwongeza mlinda mlango, Benno Kakolanya kutoka Tanzania Prisons katika kikosi chao, hali inayozidi kumweka kwenye wakati mgumu Tinoco.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here