SHARE
NA JESSCA NANGAWE

WAKATI kukiwa na tetesi za straika wa Yanga, Obrey Chirwa kutakiwa na uongozi wa Simba, Yanga wameshtukia dili na kumwita mezani nyota huyo kwa ajili ya kumalizana naye.

Chirwa amekuwa akitajwa kutakiwa na klabu ya Simba katika msimu ujao wa Ligi Kuu huku kukiwa na madai kuwa, Yanga wameshindwa kumlipa fedha zake na kutaka kiasi kikubwa cha fedha ambazo Wanajangwani hao huenda wakashindwa kuendelea naye.

Chirwa ambaye aliondoka nchini zaidi ya wiki moja iliyopita, inadaiwa alipewa ruhusa kwenda kwao Zambia kushughulikia matatizo ya kifamilia na alirejea mwishoni mwa wiki.

Hata hivyo, habari zaidi zinadai kuwa Mzambia huyo alikuwa amezisusa fedha hizo kabla ya kuitwa na kukaa meza moja na uongozi huo kujadili juu ya kiasi cha fedha anazoidai timu hiyo.

Jana Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Bonoface ‘Mkwasa’, alilithibitishia DIMBA Jumatano kuwa ni kweli starika huyo amekuwa akiwadai sehemu ya fedha zake za usajili lakini akasisitiza kuwa tayari wamekwisha…………………………….

Kwa habari zaidi usikose kununua nakala yako ya DIMBA.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here