SHARE

NA TIMA SIKILO

Beki huyo wa kimataifa wa timu ya taifa ya Uganda, anayeitumikia Azam FC, amesema yupo tayari kutua Jangwani muda wowote ikiwa ni siku chache baada ya mkali huyo kuhusishwa na kikosi cha Yanga.

Hivi karibuni baada ya mchezo wao wa Ligi Kuu kumalizika, Zahera alionekana kuzungumza kwa muda mrefu na beki huyo, hali iliyoleta minong’ono kutoka timu hizo mbili.

Dimba lilimfuata Wadada kutaka kujua kile walichoteta na kocha huyo kipenzi cha Wanajangwani na ndipo alipoweka wazi kila kitu.

Alisema kwamba, kocha huyo alimfuata na kumsifu kuhusu kiwango alichoonyesha katika mchezo huo, lakini pia akataka kujua mipango yake ya baadaye endapo atamaliza mkataba wake na Azam FC.

“Nilimwambia kuhusu kuwa na mkataba na timu yangu ya Azam na endapo kama utamalizika basi tunaweza kuzungumza,” alisema.

Mganda huyo ameweka wazi kwamba, anaweza kuitumikia Yanga, kwani yeye anafanya kazi ya kucheza soka, hivyo hachagui timu ya kuchezea ilimradi maslahi yake yanakuwa mbele.

ìNitakwenda kucheza Yanga au popote ambapo tutafikia mwafaka kulingana na mahitaji yangu”.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here