SHARE

NA JESSCA NANGAWE

Kitendo  kilichofanywa na Ibrahim Ajib kupiga mpira nje wakati anaanzisha mpira kwenye pambano la watani wa jadi, Simba na Yanga, limemshangaza kocha wake, Mwinyi Zahera.

Simba na Yanga zilikutana mwishoni mwa juma lililopita ambapo hadi kipenga cha mwisho kinalia, timu hizo zilitoshana nguvu kwa kutoka suluhu ya 0-0 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Katika mchezo huo, Ajib aliwashangaza wengi baada ya kupiga mpira nje wakati anauanzisha kitu ambacho hata kocha wake, Zahera, kinamshangaza akidai hajui nini kilimpata mchezaji wake huyo.

“Unajua ilibidi niwaulize wenzangu niliokaa nao kwamba huyu jamaa (Ajib) vipi! Maana si jambo la kawaida, unaanzisha mpira halafu unaupiga nje moja kwa moja, hata mimi nilishangaa sana.

“Labda ni mbinu yake ya mpira kuwapumbaza tu wapinzani, kwani siku zote mpira ni saikolojia lakini kiukweli binafsi nilishangaa kidogo kama wengine walivyoshangaa,” alisema.

Alisema hata Meddie Kagere wa Simba naye huwa anaziba jicho la upande mmoja kama ambavyo wanafanya wachezaji wa Liverpool, hivyo huenda hata Ajib kuna sehemu ameiga.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here