SHARE
TOPSHOT - Milan's Swedish forward Zlatan Ibrahimovic poses with his new jersey during his official presentation as new AC Milan player at the club's headquarters Casa Milan in Milan on January 3, 2020. - Ibrahimovic returns to the side on a six-month deal, promising to help rescue the struggling Serie A outfit's season. (Photo by MARCO BERTORELLO / AFP) (Photo by MARCO BERTORELLO/AFP via Getty Images)

ROME, Italia

STRAIKA mpya wa AC Milan, Zlatan Ibrahimovic, ameanza vizuri maisha yake katika timu hiyo kwa kufunga bao kwenye mchezo wa kirafiki uliomalizika kwa ushindi wa mabao 9-0 dhidi ya Rhodense.

Zlatan, 38, alitambulishwa rasmi mbele ya mashabiki wa Milan mwishoni mwa wiki hii baada ya kurejea San Siro kama mchezaji huru akitokea LA Galaxy ya Marekani.

Mabao mengine ya Milan katika mchezo huo yalifungwa na Davide Calabria, Hakan Calhanoglu, Lucas Paqueta, Rafael Leao, Samu Castillejo na Krzysztof Piatek (2).

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here